Taasisi ya kupambana na misimamo ya kuchupa mipaka inayofanya kazi chini ya Chuo Kikuu cha al Azhar cha Misri imetahadharisha kuhusu njama mbaya za Israel vamizi dhidi ya Kibla cha Kwanza cha Waislamu (Msikiti wa al Aqsa).

Tovuti ya habari ya “Rabi 21” imeripoti habari hiyo na kunukuu tamko la taasisi hiyo likisema kuwa, Masjid al Ibrahimi ni wakfu wa kila Muislamu na kwamba hata ikifanya nini Israel vamizi haiwezi kubadilisha uhakika huo. Tamko hilo limetolewa kwa mnasaba wa kukumbuka mwaka wa 28 tangu Israel ilipofanya jinai kubwa ndani ya Msikiti huo.

Chuo Kikuu cha al Azhar kimevitaka vyombo vya habari duniani kufichua jinai za Israel katika Msikiti wa al Ibrahimi na njama zake za kujaribu kuangamiza turathi za kidini na kiutamaduni za Wapalestina kwa lengo la kupandikiza siasa zake na kukigawa Kibla cha Kwanza cha Waislamu baina ya Waislamu na watu wengine kwa mujibu wa wakati na maeneo.

Taasisi hiyo imegusia jinai mbaya mno walizofanyiwa Wapalestina ndani ya Msikiti wa al Ibrahimi, mwezi 15 Ramadhani; alfajiri ya siku ya Iijumaa; iliyosadifiana na tarehe 25 Februari 1994 na kusema kuwa jinai hiyo haisameheki na haisahauliki kabisa.

Siku hiyo wakati Waislamu wakiwa Msikitini humo kwa ajili ya Sala ya Alfajiri, Musraeli mmoja anayejulikana kwa jina la Baruch Goldstein aliwavamia na kuanza kuwamiminia risasi Waislamu hao wakiwa kwenye sijda. Waislamu 29 waliuawa shahidi na makumi ya wengine kujeruhiwa katika jinai hiyo. 

Baada ya hapo Waisrael waliwashambulia na kuwaua shahidi Waislamu wengine 21 walioshiriki kwenye maziko ya Waislamu wenzao hao waliouawa kwa umati wakiwa kwenye sijda msikitini. Wapalestina wengine 50 walijeruhiwa katika shambulio hilo la pili.

(Visited 14 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!