Ingawa Timu ya Taifa ya Kandanda ya Tunisia imeshindwa kuingia kwenye hatua ya mtoano ya Mashindano ya Kombe la Dunia 2022 yanayoendelea nchini Qatar hivi sasa, lakini imetoka kibabe kwa kuwa nchi ya kwanza ya Kiarabu kuichabanga Ufaransa katika Kombe la Dunia.

Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ufaransa, umemkasirisha mkoloni huyo kizee wa Ulaya na baadhi ya wanasiasa wenye misimamo mikali ya kibaguzi wameamua kutoa maneno ya kejeli dhidi ya Tunisia.

Damien Lefebvre, mwanachama mwandamizi wa chama cha Return chenye chuki na misimamo mikali dhidi ya Waislamu na watu wa mataifa mengine ambacho kinaongozwa na mbaguzi Éric Zemmour, ameandika katika mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba: “Sawa, Watunisia tumekuruhusuni mshinde, sasa chukueni wahajiri wenu haramu.”

Damien Lefebvre ni maarufu kwa matamshi na vitendo vya chuki hasa dhidi ya Waislamu. Alikuwa msemaji wa genge lenye misimamo mikali ambalo lilipigwa marufuku mwaka 2021 kwa amri ya mahakama ya Ufaransa.

Mwanzoni mwa mwaka huu, Lefebvre alimtuhumu mshambuliaji wa Ufaransa, Karim Benzema kuwa ni gaidi na kuzusha makelele mengi. 

Miongoni mwa waliokasirishwa na tuhuma hizo za mwanasiasa huyo Mfaransa mwenye chuki na Uislamu, ni wakili wa Benzema ambaye aliandika katika Twitter kwamba: “Damien Lefebvre, mwanasiasa mwenye misimamo mikali ya kulia anachochea chuki. Katika matamshi yake ya karibuni ya Twitter amemuweka Karim daraja moja na magaidi. Je, tunapaswa kusubiri majibu mapya?”

(Visited 1 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!