Gazeti moja la kila siku la nchini Uingereza limegusia jinsi Qatar ilivyoshikamana na mafundisho ya Uislamu wakati huu ikiwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia la kabumbu na kuandika: Mwenyeji wa Kombe la Dunia ametangaza kuwa, watu wote watakaoelekea nchini humo lazima wachunge sheria rasmi za nchi hiyo.

Qatar ni nchi ya kwanza kabisa ya Waislamu na Waarabu kuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia la mpira wa miguu. Kabla ya timu za kigeni kuingia nchini humo na mashabiki wao, Qatar ilipasisha sheria hiyo na kuliarifu rasmi Shirikisho la Soka Duniani FIFA. Sheria hiyo imezingitia mafundisho ya dini tukufu ya Kiislamu.

Gazeti la kila siku la Daily Star la Uingereza limesema katika ripoti yake kwamba, serikali ya Qatar imepiga mafuruku kunywa pombe hadharani na limedai kuwa hilo ni pigo kubwa kwa mashirika ya kutengeneza pombe ambayo ndio wafadhili wakuu wa Fainali za Kombe la Dunia la kandanda.

Gazeti hilo la nchini Uingereza vile vile limedai kuwa, FIFA itapata hasara kubwa kwa kuzuia kunywa pombe kwenye viwanja vya mpira wakati wa mashindano hayo. Lakini serikali ya Qatar imesema, italipa gharama na hasara zote ili isiende kinyume na mafundisho ya Uislamu.

Fainali za Kombe la Dunia  zitafunguliwa mjini Doha Jumapili ya tarehe 20 Novemba katika Uwanja wa Michezo wa al Bayt kwa pambano baina ya mwenyeji Doha na Ecuador. Mashindano hayo yataendelea hadi tarehe 18 mwezi ujao wa Disemba, 2022.

(Visited 24 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!