Daktari mmoja wa dini ya Kihindu (Kibaniani) anayeishi nchini Canada anatumia visomo vya Qur’ani kuharakisha kupona wagonjwa wake.

Mdandao wa “The Siasat Daily” umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, Daktari Jagdish Anand Roy ni mmoja wa madaktari wa macho nchini Canada ambaye kwa miaka mingi anaendesha zahanati yake mwenyewe ya matibabu ya macho.

Jambo la kuvutia zaidi

Amma jambo la kuvutia zaidi hapa ni kwamba, ijapokuwa Dk Jagdish si Muislamu, lakini muda wote sauti ya Qur’ani Tukufu inasikika ikisomwa kwenye kliniki yake. Anapenda sana kusikiliza sura mbili za Yaasin na Ar Rahman.

Daktari baniani Canada atibu wagonjwa kwa Qur’ani
Qur’ani Kitabu Kitakatifu cha Mwenyezi Mungu

Kila anapoulizwa kuhusu sababu ya kufanya hivyo, Dk Jagdish huwa anasema, Qur’ani Tukufu ni kitabu cha wanadamu wote. Cha kuvutia zaidi huwa anasema, faida za kuweka sauti ya Qur’ani muda wote katika zahanati yake ni kwamba mazingira ya kliniki yake yanakuwa na utulivu wa aina yake, jambo ambalo linasaidia sana kupona haraka wagonjwa.

Anasemaje?

Daktari huyo wa dini ya Kibaniani pia anasema, utafiti unaonesha kuwa, mtu anaposikiliza mara tano Suratur Rahman husaidia kuondoka haraka baadhi ya maradhi ya macho. Anasema, amekuwa akiweka sauti ya Qur’ani muda wote katika zahanati yake tangu alipoianzisha. Yeye na wagonjwa wanaokwenda kwake kutibiwa huwa wanapata utulivu wa kipekee wa kimaanawi na kiroho wanapokuwa ndani ya zahanati hiiyo.

Wagonjwa wake wamelipokeaje?

Baadhi ya wagonjwa huwa wanamuuliza mbona ameweka sauti ya Qur’ani na wengine hudhani kwamba anawafanyia tablighi ya kuingia katika Uislamu. Daktari Jagdish vile vile anasema, Uislamu ni dini ya amani. Kuna wajibu wa kutofautisha baina ya Waislamu wa kweli na wale wanaotumia vibaya mafundisho ya dini hiyo. Anasema yeye anaheshimu dini zote.

(Visited 93 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!