Kanisa Katoliki duniani limelalamikia kuzidi kupungua idadi ya watu wenye hamu ya kuishi maisha ya kanisa na kushiriki katika ibada za kidini. Iwapo hali hiyo itaendelea, michango ya fedha itapungua na kanisa hilo litakumbwa na hali isiyotabirika.

Ripoti ya kila mwaka ya makanisa ya madhehebubu ya Kikatoliki iliyotolewa nchini Italia inaonesha kuwa, idadi ya wafuasi wa kanisa hilo imepungua sana, maaskofu, wachungaji,  wahubiri na makuhani pia wamepungua.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa kwenye ripoti hiyo ya kila mwaka ya Kanisa Katoliki, kuanzia mwaka 2013 aliposhika uongozi Papa Francis hadi mwaka 2018, idadi ya Wakatoliki imepungua kwa karibu watu milioni 25 duniani. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, idadi ya Wakatoliki duniani mwaka 2018 ilikuwa ni bilioni moja na milioni 328 na laki tisa na 93,000. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, idadi ya watu wote duniani mwaka huo ilikuwa ni bilioni 7.5.

Ripoti hiyo ya kila mwaka ya Kanisa Katoliki pia imesema kwamba idadi ya maaskofu, wachungaji na wahubiri wa kanisa hilo imepungua sana hasa katika mabara ya Ulaya, Amerika na Pasifiki. Ni katika mabara ya Afrika na Asia tu ndiko kunakoonekana uongezeko dogo la viongozi hao wa kanisa.

Takwimu nyingine zilizotolewa na kanisa hilo zinaonesha kwamba vituo vya chekechea vinavyosimamiwa na  taasisi za Kanisa Katoliki duniani ni 10,747, vituo vya baada ya chekechea na kabla ya shule za msingi ni 73,264 kote ulimwenguni, shule za msingi ni 103,146 na shule za sekondari ni 49,541. Taasisi hizo za elimu za Kanisa Katoliki zina wanafuzi wapatao milioni 6 kote ulimwenguni.

Hospitali zinazosimamiwa na Kanisa Katoliki kote ulimwenguni kwa mujibu wa ripoti hiyo ni 5192, maduka ya madawa ni 15481, zahanati na vituo vya matibabu ni 577, maeneo ya kuhudumia watu wazima na wenye magonjwa sugu ni 15,423 na kadhalika. Shughuli zote hizo zinatagemea misaada ya wafuasi wa kanisa hilo na ndio maana viongozi wa Kanisa Katoliki wakaelezea wasiwasi wao kwa kuona idadi ya wafuasi wake inazidi kupungua ulimwenguni.

(Visited 8 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!