Mpya Kabisa

Ginella Massa

Kwa mara ya kwanza mwanamke mwenye Hijab kuonekana mubashara runingani nchini Canada

Mwanamke wa anayevaa vazi la staha la Waislamu, Hijab, ameteuliwa kwa mara ya kwanza kabisa kuendesha kipindi mubashara katika televisheni katika historia yote ya Canada.

Vyombo vya habari vimeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, kuanzia keshokutwa Jumatatu, Bi Ginella Massa atakuwa anaongoza kipindi maalumu mubashara hewani katika televisheni ya Canada.

Kwa kweli Bi Ginella ndiye atakayekuwa mtangazaji wa kwanza kabisa katika historia kuendesha vipindi akiwa amevaa Hijab nchini Canada.

Kipindi hicho cha habari kina watazamaji wengi na ni cha televisheni ya CBC News. Kinarushwa hewani mubashara kila siku.

Mwaka 2015 pia, Bi Ginella alikuwa ripota wa televisheni ya CTV inayorusha matangazo yake kutokea Ontario na kwa kweli alikuwa ni ripota wa kwanza mwenye Hijab huko Amerika Kaskazini.

Idadi ya Waislamu inaongezeka kwa kasi katika nchi za Magharibi licha ya vizuizi vya kila namna na hii ni kwa sababu mafundisho sahihi ya Uislamu yana mvuto wa kipekee ambao unamvutia kila anayeyasikiliza kwa mazingatio.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!