Mahakama ya Katiba ya Austria imefuta marufuku ya kuvaa vazi la staha na nembo za kidini katika shule za msingi za nchi hiyo ikisisitiza kwamba marufuku hiyo ni kinyume na katiba ya nchi hiyo.

Shirika la habari la Anadolu limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, Mahakama ya Katiba ya Austria imefuta marufuku ya Hijab katika skuli za msingi za nchi hiyo iliyokuwa imewekwa  na serikali ya maadui wa Uislamu wenye misimamo mikali inayoongozwa na waziri mkuu mwenye chuki za kidini, Sebastian Kurz, mwezi Mei 2019 ikisema kuwa sheria hiyo inakinzana na katiba ya Austria.

Mkuu wa Mahakama ya Katiba ya Austria, Bw. Christoph Grabenwarter amezungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa, hukumu ya mahakama hiyo kuhusu marufuku ya kutumia nguvu na nembo za kidini katika shule za msingi nchini humo, ni kwamba marufuku hiyo inakinzana na Katiba ya Austria ya wajibu wa kuweko usawa katika mfumo wa masomo wa nchi hiyo.

Huo ni ushindi kwa Waislamu wa nchi hiyo kama ambavyo ni kufeli tena maadui wa Uislamu wenye misimamo mikali ya chuki dhidi ya Waislamu wakiongozwa na waziri mkuu wa nchi hiyo, Sebastian Kurz.

Kwa mujibu wa sheria iliyokuwa imewekwa na Sebastian Kurz na kundi lake serikalini, watoto Waislamu wa shule za msingi wenye umri wa chini ya miaka 10 walipigwa marufuku kuvaa vazi la stahala la Hijab kwa mujibu wa mafundisho ya dini yao.

Familia za watoto hao zilizokataa kuheshimu sheria hiyo iliyopasishwa Mei 15, 2019 walipigwa faini ya fedha zilizofikia hata euro 440.

(Visited 33 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!