Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu limeitaka serikali ya nchi hiyo kuimarisha ulinzi katika maeneo ya Waislamu baada ya kutiwa mbaroni majambazi wawili kwa tuhuma za kufanya wizi wa kutumia silaha katika Msikiti wa al Ihsan katika mji wa Saint Paul katika wa jimbo la Minnesota magharibi mwa Marekani.

Al Quds al Arabi imeripoti kuwa, maafisa usalama wa jimbo la Minnesota huko Marekani wamewatia mbaroni watu hao wawili baada ya kupata taarifa kuwa ndio waliofanya wizi wa kutumia silaha katika Msikiti wa al Ihsan, mjini Saint Paul.

Taarifa zinasema kuwa, majambazi hao wanaojulikana kwa majina ya Jeremy Allen Glass (32) na Christopher Edward Hughes (34), wamekamatwa na kuhusishwa na wizi wa kutumia silaha uliotokea mwishoni mwa mwezi uliopita wa Februari huko Minnesota.

Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu (CAIR) kwa mara nyingine limetoa mwito wa kuimarishwa ulinzi katika maeneo ya ibada ya Waislamu nchini Marekani ili kuepusha kujikariri uhalifu kama huo.

(Visited 1 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!