Baraza la Utafiti wa Kiislamu la Chuo Kikuu cha al Azhar nchini Misri kinaendesha mashindano ya kimataifa ya maajabu ya kisayansi ya Qur’ani Tukufu.

Hayo yameripotiwa na mtandao wa habari wa “Sada al Balad” na kuongeza kuwa, Kamati ya Maajabu ya Kisayansi ya Qur’ani Tukufu na Sunna za Bwana Mtume Muhammad SAW katika Baraza la Utafiti wa Kiislamu la al Azhar, mwaka huu pia kama ilivyojiri kwa miaka iliyopita, linafanya mashindano ya kimataifa ya maajabu ya kisayansi ya Qur’ani Tukufu na maudhui ya mashindano ya mwaka huu itakuwa ni “Maajabu ya Kisheria katika Suala la Mirathi.”

Kamati hiyo pia imesema, kuna masharti maalumu ya kutuma makala kwa sekretarieti ya mashindano hayo. Miongoni mwa masharti hayo ni kwamba makala zote lazima ziwe kwa lugha ya Kiarabu au Kiingereza, na makala yoyote ile iwe ni mara ya kwanza kuandikwa, iwe haijachapishwa wala kutumiwa sehemu yoyote ile.

Masharti mengine ni kwamba washiriki wasiwe katika wale ambao wamewahi kupata ushindi kwenye mashindano hayo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Makala zitakazotumwa zote zihusiane na maajabu ya kisayansi ya Qur’ani Tukufu katika suala la mirathi na ndani yake zitumike aya na hadithi sahihi za Mtume kwa ajili ya kutilia nguvu hoja zilizotolewa kwenye makala husika. Amma kuhusu zawadi kwa washindi wa mashindano hayo, kamati hiyo imesema, washindi watapewa zawadi zenye thamani ya hadi Pound 65 elfu wa Misri na zitatolewa kwa washindi 18. Mshindi wa kwanza atapata Pound 15 elfu, wa pili Pound elfu 10, na mshindi wa tatu atazawadiwa Pound elfu tano.

(Visited 93 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!