Mashindano ya Qur’ani Tukufu kwa ajili ya wanafunzi wa nchi za kigeni wanaosoma nchini Misri yalianza Jumatatu ya Septemba 7, 2020.

Mashindano hayo yameitishwa na Kituo cha Kiislamu cha al Azhar kwa usimamizi wa Nahla al Saeedi, mkuu wa kituo hicho kilichoko chini ya Idara ya Elimu.

Mtandao wa habari wa el Balad News umeripoti habari hiyo na kuongeza kwamba, mashindano hayo yamehusisha Hifdh na Qiraa yaani tajwidi.

Jopo la majaji wa mashindano hayo limeundwa na wataalamu na wanavyuoni wakubwa wa Qur’ani na wa fani za Qiraa na Hifdh. Lengo la mashandano hayo ni kuwahamasisha wanafunzi wa kigeni kujiidilisha kusoma vizuri Qur’ani na kuzingatia aya zake.

(Visited 50 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!