Mpya Kabisa

Masomo ya juu ya walimu wa Qur’ani yaendeshwa mtandaoni baina ya Iraq na Indonesia

Masomo daraja ya juu ya kanuni na hukmu za Qur’ani Tukufu; maalumu kwa ajili ya walimu wa Qur’ani wa kiume na kike wa Indonesia yanaendelea hivi sasa kwa njia ya Intaneti na video baina ya Iraq na Indonesia.

Mtandao wa habari za Qur’ani uitwao “dar-alquran” umeripoti habari hiyo na kusema kuwa, maustadh na maustadha wa Qur’ani Tukufu waliobobea katika fani hiyo nchini Iraq, wanatoa masomo hayo kwa njia ya Intaneti kwa walimu wa kike na kiume wa Qur’ani walioko nchini Indonesia.

Muhammad Baqir al Mansouri, raia wa Iraq aliyehifadhi Qur’ani nzima amesema, masomo hayo yanatolewa wiki mara moja na yalianza miezi miwili nyuma na yataendelea kwa muda wa miezi mitatu mingine ijayo.

Amesema, masomo hayo ni ya daraja za juu na ni maalumu kuhusu kanuni na hukmu za kusoma Qur’ani tukufu. Yanatolewa kwa watu waliofaulu masomo ya awali na ya kati ya Qur’ani Tukufu.

Kwa mujibu wa mtandao huo wa habari za Qur’ani, hadi hivi sasa walimu 350 wa Qur’ani Tukufu wake kwa waume kutoka nchi za kusini mashariki mwa Asia hasa Indonesia, Malaysia na Singapore wamepasi masomo ya Qur’ani Tukufu kutoka kwa walimu hao wa nchini Iraq.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!