Mchele mweusi ni mojawapo ya aina maalumu na za hali ya juu za mchele. Kama chakula muhimu, mchele huu una nafasi maalumu katika kitanga cha chakula cha kila kaya kote duniani….

Mchele mweusi ni mojawapo ya aina maalumu na za hali ya juu za mchele. Kama chakula muhimu, mchele huu una nafasi maalumu katika kitanga cha chakula cha kila kaya kote duniani. Nchi za Afrika Mashariki ni miongoni mwa wazalishaji wakubwa wa mchele ulimwenguni, na hicho kinahesabiwa ni kilimo cha jadi katika maeneo mengi. Lakini pamoja na hayo, mchele huu mweusi, hauonekani kuwa na soko kubwa Afrika Mashariki licha ya sifa zake nyingi za kipekee zinazoshinda mchele mweupe na wa kawahawia. Hii makala fupi itaangazia kwa muhtasari mchele mweusi katika juhudi za kuhamasisha matumizi yake.  Mwishoni mwa hii makala, nitaweka pia video ya kuonesha moja ya mapishi ya wali mweusi na jinsi baadhi ya maeneo duniani yanavyoupa umuhimu mkubwa mchele mweusi.

Mchele mweusi ni chakula katika bara la Asia tangu kale. Watumiaji wa chakula hiki barani Asia ni wengi sana. Wazalishaji wakubwa wa mchele barani Asia ni pamoja na na nchi kama Thailand, Japan, Ufilipino, Korea, India, China, Iran, Pakistan, India, Bangladesh na hata Afghanistan.

Mchele unazalishwa kwa wingi pia katika mabara ya Amerika na Ulaya. Michele nayo iko ya aina nyingine, miongoni mwake ni mchele mweupe ambao ni maarufu zaidi duniani. Lakini pia kuna mchele mweusi kama tulivyoona na wa kahawia na mwekundu. Lakini lengo la makala hii si kuangazia aina za michele, bali ni kutoa maelezo muhimu kuhusu aina moja tu ya mchele, nao ni mchele mweusi.

Mchele mweusi ni nini na sifa zake za kipekee ni zipi?

Mchele mweusi, ambao ni maarufu pia kwa jina la mchele wa zambarau kati ya baadhi ya watu duniani, ni aina maalumu na ya kipekee ya mchele. Chakula hiki kinaitwa kwa jina hilo kutokana na rangi yake inayomili zaidi kwenye rangi ya zambarau iliyokoza. Watu wa Afrika Mashariki wanajua zaidi kukhusu mchele mweupe. Baadhi ya wakati wanatumia mchele wa kahawia kwa madhumuni ya matibabu kutokana na sifa zake nyingi za kipekee, lakini kuna michele tofauti kama tulivyoeleza hapo juu, na mchele mweusi ni moja ya aina kamili zaidi, zenye lishe kamili zaidi na zenye faida nyingi zaidi za kimatibabu hasa kwa wale wasiopenda kuwa na miili minene na mafuta mingi mwilini.

Mchele huu ni chakula kilichokuwa kikitumiwa mno na jamii ya Wachina tangu karne za kale. Kutokana na sifa zake za kipekee za kimatibabu, mchele mweusi ulipigwa marufuku kuliwa na mtu yeyote asiyekuwa wa familia ya kifalme katika karne ya nne BC huko nchini China. Marufuku hiyo iliendelea kwa karne nyingi. Sababu ya kupigwa marufuku watu wasio wa familia ya kifalme kutumia mchele huo katika China ya kale, ni kwamba, kiwango cha uzalishaji wake kilikuwa kidogo sana, ladha yake ni ya kipekee na faida zake mwilini ni nyingi sana. Ni kwa sababu hiyo ndio maana mchele mweusi unajulikana pia kwa jina la mchele uliopigwa marufuku.

Kwa kuwa kwake bidhaa adimu, mchele huu hivi sasa unazalishwa katika nchi chache, na sababu yake kuu ni kwamba, watu wachache ndio wanaojua matumizi yake, namna ya uzalishaji wake na hata mapishi yake. Kwa hivi sasa mchele huu mweusi ni maarufu katika nchi kama Uchina, Ufilipino, Indonesia na Thailand, na hutumiwa kutengeneza vyakula mbali kama keki na mikate pamoja na chakula cha wali kama michele mingine.

Makala inaendelea….

Na Ahmed Rashid

(Visited 56 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!