The Sultan Qaboos Grand Mosque is the main Mosque in the Sultanate of Oman.

Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Oman imetangaza kuwa, imekusudia kufungua tena misikiti na maeneo ya ibada nchini humo lakini kwa sharti hali ya maambukizo ya corona yawe yamepungua na yawe yanaruhusu jambo hilo.

Tamko la Wizara ya Wakfu

Vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo “Middle East Affairs” vimeripoti habari hiyo na kunukuu tamko lililotolewa na Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Oman ikisema: Wizara hiyo itachukua maamuzi sahihi na mazuri kuhusu kufunguliwa tena misikiti katikati ya mwezi ujao wa Novemba (takriban mwezi mmoja na nusu ujao) kulingana na miongozo na hatua za watu wa afya za kujikinga na ugonjwa wa corona.

Taarifa ya Wizara ya Wakfu ya Oman

Wizara hiyo imeongeza kuwa, maamuzi ya kufungua misikiti yatachukuliwa kulingana na vigezo vya kieneo vilivyothibitishwa na Halmashauri Kuu na kwa sharti la kupungua idadi ya maambukizo ya COVID-19. Tayari Halmashauri Kuu ya Oman imeelezea wasiwasi wake kuhusu kuongezaeka idadi ya maambukizo na vifo vinavyotokana na ugonjwa hatari wa COVID-19 duniani. Leo Jumanne, Wizara ya Afya ya Oman imetangaza kugunduliwa kesi mpya 528 za corona na vifo vya wagonjwa 11.

Taarifa hiyo ya Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ya Oman aidha imesema: kuna wajibu wa kuchukuliwa hatua za tahadhari za kulinda roho na maisha ya watu kutokana na kuenea maambukizo ya ugonjwa wa corona na athari zake mbaya katika usalama wa umma na kuongezeka wagonjwa na vifo vinavyosababishwa na maradhi hayo.

Middle East Affairs

Wakati huo huo mtandao wa habari wa Middle East Affairs umeripoti kuwa, safari za ndege zitaanza tena siku ya Alkhamisi kwa kuchunga protokali za kiafya. Kwa mujibu wa Middle East Affairs, tarehe 18 Agosti mwaka huu, Oman iliruhusu kufunguliwa sekta ya utalii na mikahawa ya kimataifa pamoja na maeneo ya mazoezi ya mwili na mabwawa ya kuogelea katika mahoteli kwa kuchunga protokali za kiafya za kupambana na maambukizo ya kirusi cha corona.

(Visited 13 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!