Dk Nabil Luqa Bibawi, msomi wa kwanza Mkristo wa Qibti wa Misri kuchukua shahada ya Uzamivu katika Sheria ya Kiislamu, amefariki dunia.

Mtandao wa “Akhbarak” umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, Dk Nabil Luqa Bibawi ambaye ni Mkristo wa kwanza wa Qibti nchini Misri kufanikiwa kupata shahada ya Uzamivu katika Sheria ya Kiislamu, alifariki dunia Ijumaa, Februari 19, 2021.

Bibawi ameandika vitabu vingi vikiwemo vya majibu kuhusu maneno ya uongo yanayoenezwa dhidi ya dini tukufu ya Kiislamu.

Alizaliwa mwaka 1944 katika kijiji cha Bahgourah, huko Nagaa Hammadi, mkoani Qena nchini Misri. Baada ya kuchukua Diploma, alijiunga na Chuo cha Polisi na akamaliza masomo mwaka 1966. Hata hivyo aliendelea na masomo na kufanikiwa kupata shahada 8 za uzamivu katika fani mbalimbali zikiwemo za uchumi na Sheria ya Kiislamu.

“Haki na Majukumu ya Wakristo katika Nchi za Kiislamu” ndiyo iliyokuwa mada ambayo Dk Bibawi alichukulia shahada yake ya Uzamivu ya Sheria ya Kiislamu.

Alikuwa pia mhadhiri wa sheria katika Chuo cha Polisi huko Misri hadi kufariki kwake dunia.

(Visited 57 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!