Umoja wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu Duniani umeitisha mkutano wa kimataifa kwa ajili ya kujadiliana nafasi ya vyuo vikuu katika kutumikia jamii na kuzisaidia jamii hizo kutatua matatizo ya ulimwengu wa Kiislamu.

Mtandao wa habari wa Arab News umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, Umoja wa Vyuo Vikuu vya Ulimwengu wa Kiislamu umeitisha mkutano huo Jumapili ya Septemba 13, 2020 kwa njia ya Intaneti na kwa ajili ya kubadilishana mawazo na kujadiliana nafasi ya vyuo vikuu katika kutumikia jamii na kutia nguvu tunu, thamani na matukufu ya kijamii ya ulimwengu wa Kiislamu.

Osama al Abid, Katibu Mkuu wa umoja huo amesema, Muhammad bin Abdul Karim al Isa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Ulimwengu wa Kiislamu ndiye aliyetoa hotuba ya ufunguzi na katika hotuba yake hiyo ametoa maelezo kuhusu nafasi ya vyuo vikuu katika kuimarisha na kutia nguvu mshikamano wa kijamii.

Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Ulimwengu wa Kiislamu pia amesema, vyuo vikuu vya Kiislamu vina nafasi muhimu katika utatuzi wa matatizo mengi yaliyopo duniani leo na si ya ulimwengu wa Kiislamu tu.

Miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na namna ya kustafidi vizuri na teknolojia za kisasa katika ulimwengu wa Kiislamu, kukabiliana na aidiliojia za misimamo mikali ambayo haikufundishwa na Uislamu na pia athari kubwa za ugonjwa wa COVID-19 katika mabadiliko ya mbinu na njia za usomeshaji na usambazaji elimu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!