Mpango wa kujengwa Msikiti mkubwa zaidi huko kaskazini magharibi mwa Uingereza, umepasishwa na Baraza la Mji wa Blackburn.

Mtandao wa habari wa Arab News umeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, mradi huo mkubwa utaendeshwa na ndugu mabilionea wanaomiliki maduka makubwa ya Asda. Licha ya kukumbwa na upinzani mkubwa, lakini hatimaye mpango huo umepasishwa na baraza hilo la mji wa Blackburn huko Uingereza.

Paul Browne, mshauri katika chama cha Liberal Democrat cha Uingereza ni miongoni mwa wapinzani wa mradi huo. Katika hotuba yake mbele ya Baraza la Mji wa Blackburn, Browne amesema, minara mirefu na sauti za Adhana ni miongoni mwa mambo yasiyopendeza – kwa mtazamo wake – katika mradi huo.

Hata hivyo mkuu wa mipango ya ufanikishaji wa mradi huo amesema kuwa, minara ya Msikiti huo haitapindukia mita 29 kwenda juu. Gavin Prescott amesema, minara hiyo haitokuwa mirefu zaidi ya minara ya makanisa mawili yaliyopo karibu na eneo utakapojengwa Msikiti huo. Pia amesema, sauti ya adhana nayo itapunguzwa.

Gharama za ujenzi wa Msikiti huo mkubwa zaidi huko magharibi mwa Uingereza imekadiriwa kufikia Pound milioni tano (5,000,000) sawa na dola milioni 6.9 za Kimarekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!