Klaus von Stosch, mhadhiri na mtaalamu wa dini katika Chuo Kikuu cha Cologne cha Ujerumani anaamini kwamba Qur’ani Tukufu imetoa ufafanuzi mzuri kuhusu Bibi Maryam SA mama wa Masih Isa AS na imemtaja kuwa bibi huyo alikuwa mtukufu na msafi ikiwa ni kupambana na maneno machafu yaliyokuwa yanatolewa kuhusu bibi huyo mtukufu.

Mhadhiri huyo wa chuo kikuu amezaliwa mjini Cologne na amepata elimu yake katika Chuo Kikuu cha Freiburg huko Bonn, Ujerumani. Mada aliyosomea kwa kina ni Theology ya Kikatoliki.

Tangu mwaka 2008, Stosch anasomesha katika Chuo Kikuu. Muda wote anaweka maelezo za maudhui tofauti na mijadala baina ya dini mbalimbali katika tovuti yake na analenga zaidi kwenye mambo ambayo yanazikutanisha pamoja dini zinazojinasibisha na Nabii Ibrahim AS.

Watu mbalimbali wamevutiwa na tovuti hiyo. Ameamua pia kuanzisha taasisi ya CTSI mjini Bonn kwa ajili ya mijadala ya kimataifa kuhusu dini tofauti. Taasisi hiyo imepangwa kufunguliwa rasmi mwezi huu wa Mei.

Anasema, Qur’ani inaweza kutumika kutoa ufafanuzi mzuri kuhusu Ukristo. Amesema, kuukosoa Ukristo ni jambo lisiloepukika kwani dini hiyo imeelekea upande ambao unaifanya itumiwe kwa malengo ya kisiasa na madola ya kibepari na hilo ni tishio kwa Ukristo. Kuna hatari pia ya kumtumia vibaya Masih Isa AS, lakini aya za Qur’ani zimeashiria wazi hatari hiyo na kuwatahadharisha watu wasijitumbukize kwenye shimo hilo.

(Visited 33 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!