Uingereza imemuenzi na kuthamini mchango wake, mwanafizikia wa kwanza kabisa Muislamu kushinda tunzo ya fizikia ya Nobel.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Sputnik, Idara ya Mirathi ya Uingereza imeweka jina la Muhammad Abdus Salaam, raia wa Pakistan katika bango la kumbukumbu la nchi hiyo linalojulikana kwa jina la ”Bango Buluu” ambalo ndani yake kila mwaka huwa kunaandikwa majina ya watu muhimu na wakubwa, waliotoa huduma muhimu duniani kama njia ya kuwaenzi.

Katika ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Twitter, idara hiyo imeandika, bango lenye picha ya Abdus Salaam, limewekwa pembeni mwa Bango Buluu, ikiwa ni nembo ya kihistoria kwa ajili ya kutukuza watu muhimu na wakubwa duniani.

Idara ya Mirathi ya Uingereza imeandika: Bango Buluu mwaka huu limepambwa kwa jina la msomi mkubwa wa fizikia aliyeishi kuanzia mwaka 1926 hadi 1996.

Katika ujumbe wake mwingine wa Twitter, idara hiyo imeandika, Abdus Salaam amejiunga na wasomi wakubwa ambao majina yao daima yamekuwa yakiandikwa katika Bango Buluu.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza pia imeandika katika ukurasa wake rasmi wa Twitter kwamba, Profesa Abdus Salaam alikuwa mwanafizikia mkubwa ambaye alitoa huduma kubwa kwa nchi zinazoendelea kutokana na ilhamu aliyopata kutoka katika dini yake yaani Uislamu.

Wizara hiyo imeongeza kuwa, Idara ya Mirathi ya Uingereza imeamua kuliingiza jina la msomi huyo mkubwa Muislamu katika orodha ya wasomi wa Bango Buluu kutokana na kwamba Abdus Salaam alikuwa Muislamu wa kwanza kabisa kupata tunzo ya fizikia ya Nobel. Profesa Abdu Salaam raia wa Pakistan alitunukiwa tunzo na fizikia ya Nobel mwaka 1979 kutokana na utafiti aliofanya na kuja na nadharia ya fizikia kuhusu seli shina, nadharia ambayo hadi leo inatumika duniani.

(Visited 25 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!