Baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa Bunge la Uholanzi, imebainika kuwa mmoja wa walioshinda katika uchaguzi huo ni mwanaharakati Muislamu anayevaa Hijab.

Kwa mujibu wa “The New Arab” mwanaharakati huyo wa masuala ya mazingira anajulikana kwa jina la Bi Kauthar Bouchallikht.

Mwanaharakati huyo ana asili ya Morocco na amechaguliwa kukiwakilisha Bungeni chama cha Groen Links.

Kabla ya uchaguzi huo, vyama vyenye chuki na wageni nchini Uholanzi vilieneza chuki kubwa dhidi ya mwanaharakati huyo vikidai ana chuki na Mayahudi.

Alipohojiwa na gazetila Glamor, Bi Kauthar amesema, kuna watu wengi nchini Uholanzi wanafanya njama za kuihusisha dini yangu ya Kiislamu na vitendo vya kigaidi na mara nyingi hushangaa wanapomuona mwanaharakati wa kike Muislamu anayechunga vazi la staha la Hijab akiwa mstari wa mbele kutetea mazingira.

Amesema, ninaamini kwamba ardhi ni zawadi tuliyopewa na Mwenyezi Mungu na ni wajibu wetu kuitunza vizuri.

Uchaguzi wa Bunge la Uholanzi ulifanyika tarehe 15 hadi 17 Machi 2021 kwa kuchungwa protokali zote za kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19. Matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi huo yanaonesha kuwa, chama cha Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Demokrasia kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa serikali ya mpito, Mark Rutte kimepata ushindi wa viti vingi kwenye uchaguzi huo.

(Visited 33 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!