Shirika la kijasusi la Shirikisho la Russia limetangaza habari ya kutiwa mbaroni raia mmoja wa nchi hiyo mwanachama wa genge la kigaidi lenye misimamo mikali la Ukraine aliyekuwa amepanga kuuripua kwa mabomu Msikiti mmoja katika Jamhuri ya Altai, magharibi mwa Siberia huko Russia.

Televisheni ya “Rusia al Yaum” imetangaza habari hiyo na kuzinukuu duru hizo za kijasusi za Shirikisho la Russia zikiongeza kuwa, raia mmoja wa Russia, mwanachama wa genge (la kigaidi) lenye misimamo mikali la Ukraine alikuwa na nia ya kufanya operesheni za kigaidi kwenye maeneo ya Kiislamu ukiwemo Msikiti mmoja katika Jamhuri ya Altai ya magharibi mwa Siberia, lakini ametiwa mbaroni.

Vyombo vingine vya habari vya Russia vimelinukuu shirika la kijasusi la shirikisho la nchi hiyo likisema kuwa, gaidi huyo amezaliwa mwaka 2000, ni mwanachama wa genge la kigaidi la “Mjumuiko wa Kitaifa wa Ukraine” na ana uraia wa Russia. Ametiwa mbaroni katika mji wa Barnaul wa Jamhuri ya Altai, magharibi mwa Siberia nchini Russia.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, gaidi huyo amekiri kwamba alipanga kufanya operesheni za kigaidi za moja kwa moja dhidi ya mikusanyiko ya Waislamu na taasisi za serikali ili kuzusha hofu katika nyoyo za wananchi hasa Waislamu wa Asia ya Kati. Baada ya kupata taarifa za kiintelijensia, maafisa usalama wa Russia wamewahi kuivamia nyumba ya kijana huyo na kugundua mada za miripuko na machapisho ya kuchochea chuki hasa dhidi ya Waislamu na pia picha za maeneo ambayo magaidi hao walipanga kuyashambulia.

(Visited 40 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!