Makumbusho ya Kiislamu nchini Australia, ni kivutio cha kipekee kutokana na mvuto wa jengo lake kabla ya jambo lolote lile. Jengo hilo liko katika eneo la Thornbury jijini Melbourne, Victoria, kusini mashariki mwa Australia.

Awali kabisa pendekezo la kujengwa jengo hilo lilitolewa mwaka 2010 na taasisi moja isiyo ya kiserikali kwa gharama ya dola zifikazo milioni 10. Mchoro ulitolewa mwaka 2014.

Serikali ya Australia haikuwa tayari kutoa fedha zote hizo kugharamia ujenzi wa makumbusho hayo ya Kiislamu. Hata hivyo Waislamu wenye ghera na dini yao walijitolea asilimia 80 ya ujenzi wa makumbusho hayo muhimu baada ya serikali ya Australia kugharamia asilimia 20 tu ya ujenzi wake.

Jengo la Makumbusho ya Kiislamu nchini Australia lina maeneo mengi ya maonyesho na yamegawanywa katika vipengee tofauti vinavyohusiana na utamaduni na ustaarabu wa Kiislamu.

Eneo moja la maonyesho ndani ya jengo hilo ni maalumu kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu misingi ya dini ya Kiislamu kama vile Shahada, Sala, Funga, Zaka, Hija, Jihadi n.k. Katika sehemu hiyo kumetolewa ufafanuzi sahihi wa sheria za Kiislamu hasa masuala kama Jihadi ili kufuta propaganda potofu zinazoenezwa kuhusu mafundisho matukufu ya Uislamu na istilahi zake. Watembeleaji wa eneo hilo wanaweza kusimama kwenye mnara uliowekwa kwenye eneo hilo na kusikiliza adhana.

Maelezo kuhusu sira na maisha ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na maeneo waliyoishi ikiwemo sira ya Mtume Muhammad SAW, turathi za uvumbuzi wa aina yake uliogunduliwa na wasomi Waislamu katika masuala ya kisayansi, hisabati na fasihi ni uwanja mwingine uliopewa kipaumbele kwenye jengo la Makumbusho ya Kiislamu nchini Australia.

Eneo jingine la makumbusho hayo ni maalumu kwa ajili ya kuonesha kazi za wasanii Waislamu wa nchini Australia.

Katika eneo linalohusiana na itikadi za Kiislamu, kuna sehemu ya kuonesha ibada na amali za kivitendo ndani ya Uislamu kama Hija na kutufu Alkaaba. Hapa chini tumeweka kipande cha video kuhusu jengo hilo la Makumbusho ya Kiislamu la huko kusini mashariki mwa Australia ambalo kabla ya jambo lolote, muundo wake wa kipekee wa uhandisi wa kisasa, ni kivutio cha watalii wengi nchini humo.

Hapa chini ni kipande cha video kuhusu makumbusho hayo

Na hapa chini ni baadhi ya picha za makumbusho hayo

(Visited 54 times, 1 visits today)
One thought on “Picha na Video: Jengo la Makumbusho ya Kiislamu, kivutio cha kipekee Australia”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!