Msikiti wa Fatimatuz Zahra (AS) wa nchini Kuwait, ambao ni maarufu kwa jina la Taj Mahal ya Mashariki ya Kati, ni katika majengo yenye mvuto wa kipekee kwenye eneo la Asia Magharibi.

Msikiti huo uko katika mji wa Kuwait City (mji mkuu wa Kuwait) na uhandisi majengo uliotumika ndani yake unamvutia kila anayepita karibu na eneo hilo. Msikiti huo unafanana sana na jengo la kihistoria la Taj Mahal la nchini India. Msikiti huo ni maarufu kwa jina la Taj Mahal ya Kuwait.

Ujenzi wa Msikiti huo ulianza mwaka 2008 na ulimalizika mwaka 2011. Msikiti huo una uwezo wa kupokea Waislamu 4000 kwa wakati mmoja. Minara minne ya Msikiti huo ina urefu wa mita 33. Kuba lake ni moja na lina upana wa mita 16 na urefu wa mita 22. Vyote hivyo vimejengwa kwa ustadi wa hali ya juu kabisa.

Mawe ya marmar yaliyotumika kujengea Msikiti huo yametokea Uajemi (Iran) na wataalamu kutoka Uajemi na India walishirikiana kuchonga mawe hayo kwa muda wa miezi minane (8) na kuwezesha kutumiwa katika ujenzi wa Msikiti huo. Karibu na Msikiti huo wa Fatimatuz Zahra pamejengwa maktaba na kituo cha mikusanyiko ya Waislamu ambacho kina sehemu za wanaume mbali na wanawake mbali. Eneo la kugeshea magari la Msikiti huo lina uwezo wa kupokea magari 1000 kwa wakati mmoja.

Hapa tumeweka video fupi ya Msikiti huo

Hapa chini tumeweka baadhi ya picha za Msikiti huo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!