Ujenzi wa Msikiti na kituo kipya cha Kiislamu unaendelea katika mji wa East Brunswick wa jimbo la New Jersey nchini Marekani.

Kwa mujibu wa tovuti ya “Tapinto” uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho kipya uliofanyika siku chache zilizopita ulihudhuriwa na Meya wa mji wa East Brunswick pamoja na Waislamu wa matabaka mbalimbali.

Msikiti na kituo hicho kipya cha Kiislamu kitajumuisha sehemu ya ibada na ya kusalia pamoja na madrasa na ofisi nyinginezo mbalimbali za kushughulikia masuala ya Waislamu.

Faheem Soherwardy, Mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha East Brunswick amesema, kituo hicho kitakuwa na sehemu ya kufanyia ibada Waislamu, kusoma elimu za kidini, shughuli mbalimbali za Waislamu na pia kukaribisha wakazi wa mji huo katika minasaba tofauti inayochunga mafundisho ya Kiislamu.

Amesema, ana matumaini kwamba baada ya kuondolewa sharia kali za corona, kituo hicho kitakuwa pia mwenyeji wa vikao mbalimbali vya watu wa dini tofauti kwa ajili ya kulinda na kupigania haki za wakazi wote wa mji wa East Brunswick huko New Jersey, Marekani.

Kwa upande wake, Meya wa mji wa East Brunswick, Brad Cohen, amesema: “Ninaunga mkono kujengwa Msikiti mpya katika mji wetu na ninamuomba Mwenyezi Mungu awape afya njema, ustawi na awazidishie mapenzi Waislamu.” Mji wa East Brunswick una wakazi takriban 47,000. Shughuli za kituo cha Kiislamu katika mji huo zilianza mwaka 2004 nje ya kanisa moja dogo lililokarabatiwa.

Hapa chini tumweka baadhi ya picha za uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!