Gazeti la New York Times la nchini Marekani limeripoti kuwa, polisi wa Ufaransa wamevamia nyuma nne za watoto Waislamu na kuamiliana nao kama magaidi baada ya watoto hao kuwaambia walimu wao shuleni kuwa wanavichukia vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.

Televisheni ya al Jazeera ya Qatar imelinukuu gazeti hilo la Marekani likiandika kwamba, tarehe 5 Novemba, 2020, wanajeshi wa Ufaransa walivamia nyumba 4 za wanafunzi hao wa shule ya msingi katika mji wa Albertville mapema asubuhi ya siku hiyo na kuamiliana na watoto hao kama magaidi licha ya umri wao mdogo wa miaka 10. Watatu kati ya watoto hao wana asili ya Uturuki na mwingine asili yake ni Algeria.

Hayo yametokea baada ya skuli ya Louis Pasteur kuwashitaki watoto hao kwa kudai kuwa watoto hao wamewaambia walimu wao kwamba wanachukizwa na vikatuni vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW baada ya kuulizwa maswali na walimu wao.

Baada ya kuwasilishwa mashtaka hayo, jeshi la polisi la Ufaransa liliuhesabu msimamo wa watoto hao Waislamu kuwa ni kuunga mkono ugaidi, wakatoa amri ya kuvamiwa nyuma zao na kuwateka watoto hao wadogo kama wanavyoteka magaidi, wakawanyanyasa na kuamiliana nao kama wahalifu wa ugaidi na kuwasaili kwa muda wa masaa 11 katika kituo cha polisi. Kumezuka wimbi la hasira kubwa za Waislamu wa Ufaransa kama ambavyo uovu huo wa polisi wa Ufaransa umelaaniwa katika nchi mbalimbali za Waislamu duniani, baada ya kuenea picha za polisi wa Ufaransa katika mitandao ya kijamii zinazowaonesha wakivamia nyumba za watoto hao.

Watoto hao hadi hivi sasa wameathirika kisaikolojia.

(Visited 90 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!