Kundi la watu wwenye siasa kali waanaojiita wapenda utaifa nchini Uturuki wameshambulia kanisa la Warmenia mjini Istanbul na baadaye wamepanda juu ya kanisa hilo, wakaanza kupiga muziki na kucheza. Jambo hilo limelaaniwa vikali na viongozi wa Uturuki wakiongozwa na Rais Recep Tayyip Erdogan.

Kwa mujibu wa Rusia al Yaum, Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amelaani kitendo cha kundi hilo la watu wenye misimamo mikali cha kushambulia kanisa la Kiarmenia na kupanda juu ya jengo la kanisa hilo la Sorp Takafor mjini Istanbul na kupiga muziki na kucheza.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, serikali ya Uturuki imeshawatia mbaroni watu kadhaa kwa kosa hilo. 

Tovuti ya habari ya Russia al Yaum imeweka pia kipande cha video kinachowaonesha watu hao waliokuwa wamelewa, wakiwa juu ya jengo la kanisa hilo wakipiga muziki na kucheza.

Ikumbukwe kuwa, uhusiano wa Uturuki na Armenia si mzuri huku Waarmenia wakilalamika kuwa, Waturuki walifanya mauaji ya umati dhidi ya jamii ya Waarmenia mwaka 1915. 

Uturuki inakanusha kuhusika wafalme wa Uthmania (Ottoman Empire) katika mauaji hayo. Hata hivyo suala hilo linatumiwa mara kwa mara kuchochea ugomvi baina ya pande hizo mbili. 

Viongozi wa Uturuki wanasema kuwa, walioshambulia kanisa la Waarmenia mjini Istanbul, wana nia ya kuzusha fitna mpya baina ya Uturuki na Armenia.

(Visited 26 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!