Ramadan muslim islam drawing (Religion) ramadan,muslim,islam,religion,arabic,eid

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni muhimu mno kwa Waislamu. Hata hivyo mwaka huu pia ugonjwa wa COVID-19 umeendelea kuathiri ibada za Waislamu ndani ya Ramadhani. Waislamu wanaendelea na ibada ya funga na ibada nyinginezo ndani ya mwezi huu wakichunga protokali za watu wa afya kwa ajili ya kuepusha maambukizo ya corona. Utukufu wa Ramadhani umevigusa pia vyombo vya habari vya Magharibi ambavyo vimelazimika kuakisi ibada na a’amal za Waislamu ndani ya mwezi huu mtukufu. Vyombo mbalimbali vya Magharibi vinaakisi kwa nyakati tofauti ibada, ada na desturi za Waislamu wa maeneo tofauti ulimwenguni wakati wa Ramadhani. Miongoni mwa vyombo hivyo ni televisheni ya CNN ya Marekani ambayo katika ukurasa wake wa Intaneti imeweka picha mbalimbali na kuandika makala kuhusu a’amal, ibada ada na desturi za Waislamu wa maeneo tofauti duniani, na jinsi vyombo mbalimbali vya habari vya Magharibi vilivyoakisi siku za mwanzoni mwa Ramadhani ya 1442 (2021). Hapa chini tumeweka baadhi ya picha hizo.

Hapa chini tumewekwa baadhi ya picha na maelezo kwa ufupi

Sala wakati wa Ramadhani katika Msikiti wa al Farouq Umar, Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).
Sala ya jamaa baada ya futari ya Ramadhani katika Msikiti wa Massalikul Jinaan, mjini Dakar, Senegal.
Utengenezaji na upikaji wa tambi mjini AllahAbad India. Tambi hizo zinatumiwa kupikia chakula kitamu cha jadi, maalumu kwa ajili ya Ramadhani. Kinapendwa na kutumiwa sana na Waislamu wa India. Chakula hicho kinaitwa Siwaiyan (Seviyan) na ni aina fulani ya halua inaliwa zaidi wakati wa daku, lakini zaidi siku ya sikukuu ya Idul Fitr na Waislamu wa kona zote za India.
Sala ya Magharibi katika Msikiti wa al Azhar, mjini Cairo Misri.
Waislamu katika mgodi wa makaa ya mawe wakisoma dua wakati wa daku nchini Uturuki.
Sala katika Kituo cha Kiislamu mjini Washington Marekani, wakati huu wa Ramadhani.
Usomaji wa Qur’ani ni katika ibada kubwa za mwezi wa Ramadhani. Hapa Waislamu wakisoma Qur’ani ndani ya mwezi huu wa Ramadhani katika Msikiti Mkuu wa Umari, Ukanda wa Ghaza huko Palestina.
Ada na desturi ya Waislamu wa Bosnia mjini Herzegovina ya kufyatua mizinga kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Sala ndani ya Ramadhani ya 1442 (2021) katika Msikiti mmoja wa Zagreb, mji mkuu wa Croatia.
Muda mchache kabla ya futari katika soko moja la Nablos, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, Palestina katika siku za mwanzoni mwa Ramadhani ya mwaka huu 1442 Hijria, 2021 Milaadia.
(Visited 63 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!