Kwa mwaka wa pili mfululizo, Sala ya Idul Adh’ha inatarajiwa kusaliwa katika uwanja mkubwa wa michezo katika mji mkuu wa Ireland, Dublin, wiki ijayo

Kwa mujibu wa Irish Times, Waislamu wa Ireland, mwaka huu pia watatekeleza ibada ya Sala ya idul Adh’ha kaika uwanja mkubwa wa michezo wa mji mkuu Dublin, ujulikano kwa jina la Croke Park. 

Waislamu 500 wanaweza kushiriki katika ibada hiyo ya Sala. Mwaka jana Waislamu 200 tu ndio walioruhusiwa kutekeleza ibada hiyo katika uwanja wa Croke Park kutokana na sheria kali za kujikinga na ugonjwa hatari wa COVID-19.

Sheikh Umar al Qadri, Mkuu wa Baraza la Kiislamu la Waislamu wa Ireland la Amani na Mshikamano na ambaye ndiye anayesimamia ibada hiyo amesema kuwa, kila mtu anaweza kujiandikisha mapema kwa ajili ya kuruhusiwa kushiriki katika Sala hiyo kutokana na kuwa, si kila mtu atapata fursa ya kushiriki kutokana na sheria kali za corona. Vituo vya kujiandikisha vimewekwa Belfast, Portlaoise, Athlone, Dublin, na mtu anaweza kushiriki kutoka sehemu yoyote ile. “Hiyo ni ibada ambayo kila mtu atapenda kushiriki,” amesema, Sheikh al Qadri.

 Wanaopenda kushiriki katika ibada hiyo tukufu wanaweza kujiandikisha pia mtandaoni kwenye tovuti ya eventbrite.ie

(Visited 1 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!