Adhana ya zamani kabisa kuwahi kurekodiwa katika Msikiti Mtakatifu wa Makkah (Masjid al Haram) ni hii yenye umri wa takriban karne moja na nusu, miaka 140. Adhana hiyo ilirekodiwa na mtaalamu wa masuala ya mashariki mwa dunia, raia wa Uholanzi.

Mtandao wa AJEL wa Saudi Arabia umeripoti habari hiyo na kuweka kipande cha sauti ya Adhana iliyorekodiwa katika Msikiti Mtakatifu wa Makkah na mtaalamu wa masuala ya mashariki mwa dunia raia wa Uholanzi aliyejulikana kwa jina la Christiaan Snouck Hurgronje. Aliirekodi adhana hiyo mwaka 1885 Milaadia, iliyosadifiana na mwaka 1302 Hijria.

Kumbukumbu hiyo ya aina yake, hivi sasa inahifadhiwa katika Chuo Kikuu cha Leiden nchini Uholanzi. Hata hivyo jina la Mwadhini halijukutajwa.

Christiaan Snouck Hurgronje ametunga pia kitabu kiitwacho “Kurasa za Historia ya Makkah” na ndani yake mna maelezo kuhusu safari yake ya Jeddah na Makkah huko Hijaz (Saudi Arabia) mwaka 1882 na 1885. Alifanyia utafiti mkubwa pia nafasi ya Hija kwa Waislamu na umuhimu wake katika Uislamu. Hapa chini tumeweka sauti ya Adhana hiyo ya karibu karne moja na nusu iliyopita kama ilivyoripotiwa na mtandao huo wa AJEL wa nchini Saudi Arabia.

Adhana ya zamani kabisa kurekodiwa katika Msikiti wa Makkah. Ina umri wa takriban karne moja na nusu miaka 140
(Visited 90 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!