Rais wa wa Chuo Kikuu cha al Azhar ch Misri maarufu kwa jina la Shaykhul Azhar ametoa amri ya kutumiwa mfuko wa Zaka na Sadaka kuwafikishia misaada ya haraka ya chakula, matibabu na mahitaji mengine, watu walioathiriwa na mafuriko nchini Sudan.

Toleo la mtandaoni la gazeti la al Ahram la Misri limemnukuu Sheikh al Azhar; Sheikh Ahmad al Tayyib akitoa amri hiyo kwa maafisa wa Kitengo cha Zaka na Sadaka cha Misri kushirikiana na maafisa husika wa Chuo Kikuu cha al Azhar, kuwafikishia misaada ya haraka ya chakula, madawa na mahitaji mengine, watu walioathiriwa na mafuriko huko Sudan.

Idadi ya watu waliofariki duniani nchini Sudan kutokana na mafuriko imeongezeka kutoka 80 siku chache zilizopita hadi zaidi ya 112 huku kukiwa na hofu ya kuongezeka zaidi idadi ya wahanga wa janga hilo la kimaumbile.

Nyumba 83440 huku 34,944 zikiharibiwa kikamilifu. Maeneo 413 ya huduma za umma na maduka 108 yameharibiwa huku zaidi ya vijiji 250 vya kaskazini, katikati na magharibi mwa Sudan vikiwa vimeathiriwa na mvua kubwa zinazonyesha kwa mwezi mzima sasa. Hayo ni kwa mujibu wa Baraza la Taifa la Ulinzi wa Raia la Sudan.

Hivi karibuni Kitengo cha Zaka na Sadaka cha Misri kilipeleka misaada mingi ya kibinaadamu kwa waathiriwa wa mafuriko huko Sudani vikiwemo vyakula, mablanketi na vifaa vya tiba na madawa. 

Mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi mwaka huu yamesababisha mafuriko makubwa katika nchi mbalimbali duniani kama vile Afghanistan, Pakistan, Sudan, Chad n.k.

Uharibifu katika baadhi ya nchi ni mkubwa kiasi kwamba hata kufikisha misaada ya kibinadamu ni shida sana. Viongozi wa Pakistan kwa mfano wameyaomba mataifa ya dunia hasa nchi za Waislamu kuisaidia kukabiliana na maafa ya mafuriko baada ya kulemewa na ukubwa wa maafa hayo.

(Visited 18 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!