Picha ya kwanza

Tarehe 5 Agosti 1990 jumuiya ya OIC iliainisha siku maalumu ya haki za binadamu kwa mtazamo wa dini tukufu ya Kiislamu.

Siku hiyo inakumbusha tukio la kupasishwa Azimio la Haki za Binadamu katika Mtazamo wa Kiislamu kwenye mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) tarehe 5 mwaka 1990. Siku hiyo nchi za Kiislamu, kwa mara ya kwanza kabisa, zilitangaza mitazamo ya Kiislamu kuhusu haki za binadamu na majukumu ya serikali katika hati inayoshabihiana na nyaraka za haki za binadamu na za kisheria za kimataifa. 

Tajiriba na uzoefu vinaonyesha kuwa, haki za binadamu si suala la opande mmoja kuutwisha upande au jamii nyingie, bali kila kaumu au taifa na dini inaarifisha na kuainisha haki za binadamu kwa msingi wa mafundisho na muiundo ya kiutamaduni, kijamii na dini yake. Ni wazi kuwa, mtazamo wa haki za binadamu unapaswa kujiepusha na masuala ya kisiasa na ubainishe thamani halisi za binadamu bila ya kijali mbari, rangi na utaifa maalumu. Kwa sasa msingi wa haki za binadamu za kimataifa ni Azimio la Kimataifa za Haki za Binadamu lililopasishwa Disemba mwaka 1948 katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Kifungu cha kwanza cha azimio hilo kimeashiria mambo makuu matatu ambayo ndiyo msingi wa haki za binadamu. Misingi hiyo ni uhuru, usawa na udugu. Hata hivyo inasikitisha kusema kuwa, hata misingi hii mikuu mitatu ya Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu inakanyagwa na kupuuzwa na waliobuni azimio hilo.

Hivyo na kutokana na sababu kadhaa baadhi ya nchi duniani ziliamua kubuni hati na maazimio ya haki za binadamu yanayooana na utamaduni, maadili na itikadi zao za kijadi. Vilevile itakumbukwa kuwa, baada ya Umoja wa Mataifa kuutangazia ulimwengu Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu mwaka 1948, nchi nyingi za dunia zilitangaza kuwa, haki hizo zimeandikwa kwa mujibu wa misingi ya kiliberali na kisekula ya Magharibi na kwamba sheria hizo haziendani na utamaduni wa nchi hizo hususan zile za Kiislamu.   

Hivyo kulijitokeza tofauti katika kuarifisha haki halisi za binadamu. Kuna sababu kuu tatu zilizopelekea kujitokeza hitilafu hizo. Kwanza ni kuwa, haki za binadamu kwa mtazamo wa upande mmoja wa nchi za Magharibi, kivitendo, zimekuwa fimbo na wenzo wa mashinikizo dhidi ya nchi nyingine. 

Sababu ya pili ni kuwa, haki za binadamu katika dunia ya sasa zinatokana na mitazamo ya Kimagharibi ambayo aghlabu ina sura ya kisiasa. Na tatu ni tofauti za kimsingi baina ya mtazamo wa kimaada wa Magharibi na mtazamo wa kiroho na kimaadili kuhusiana na haki za binadamu. Kwa mfano tu tunaweza kuashiria baadhi ya haki zinazohusiana na uhai wa binadamu kama haki ya kupinga ukoloni na kupambana nao, haki ya kukabiliana na uvamizi na tishio lolote dhidi ya uhai wa binadamu, na haki ya mwanadamu kuishi katika mazingira salama na yaliyojitenga na ufuska na vilevile haki ya kuwa na usalama wa kidini ambavyo vimepuuzwa katika Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu. Inasikitisha kusema kuwa, matukio mengi ya kusikitisha yanayojiri kila siku katika pembe mbalimbali za dunia ni matokeo ya mitazamo ya kisiasa iliyojificha ndani ya azimio la haki za binadamu lililobuniwa kwa msingi wa mitazamo ya kiliberali ya nchi za Magharibi. Ukweli huu unashuhudiwa vyema zaidi katika mieneno isiyo ya kibinadamu ya Marekani katika nchi mbalimbali.

Kwa hisani ya PARSTODAY

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!