Maafisa wa Indonesia wamewatia mbaroni watu 6 kwa tuhuma za kuvunjia heshima matukufu ya Uislamu kupitia kueneza ufuska wa kunywa pombe nchini humo kwa jina la Uislamu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP kama lilivyonukuliwa na tovuti ya Barrons, watu hao wametiwa mbaroni kwa kuendesha kampeni ya kilabu cha pombe lakini baya zaidi ni kwamba, walikuwa wametenga kila siku ya Alkhamisi kumpa chupa ya bure ya pombe kila Muislamu mwenye jina la Muhammad au Maria yaani Maryam.

Kuwa Muislamu lilikuwa moja ya masharti ya kupewa chupa ya pombe kila Alkhamisi ambayo ndiyo yenye usiku wa kuamkia Ijumaa ambayo ni siku tukufu na muhimu kwa Waislamu kila wiki.

Maadui wa Uislamu wanafanya kila njia kuhakikisha Waislamu hawaishi kwa utulivu. Kama maadui hawa wamefanya kwa makusudi kutumia jina la Muhammad na Maryam kutangaza pombe katika siku ya Alkhamisi ya kuamkia Ijumaa ambazo ni siku muhimu sana kwa Waislamu

Kampeni hiyo ambayo sasa imefutwa, ilijulikana kwa jina la Holywings. Jana Ijumaa, polisi wa Indonesia waliwatia mbaroni watuhumiwa hao sita wakiwemo wakuu wa kampeni hiyo pamoja na mkuu wa timu nzima ya klabu ya pombe iliyoanzisha kampeni hiyo.

Watuhumiwa wote sita wamevishwa sare za jela za rangi ya chungwa, ikiwa na maana kwamba, makosa yao ni ya kijinai na kama watapatikana na hatia basi wanaweza kufungwa miaka 10 jela kila mmoja.

Waislamu wa Indonesia walilalamikia vikali ufuska huo kiasi kwamba wakuu wa kilabu hiyo ya pombe walilazimika kuomba radhi na kudai kuwa wao kama viongozi hawakuwa na taarifa ya kufanyika jambo hilo. Ijapokuwa sheria za Indonesia hazipigi marufuku pombe, lakini wananchi wa nchi hiyo ni Waislamu wanaoheshimu mafundisho ya dini yao na kunywa pombe ni nadra kwa raia wa asili wa Indonesia.

(Visited 19 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!