Serikali ya Ufaransa imeamua kufunga Misikiti mingine 6 ikiwa ni muendelezo wa vitendo vyake vya chuki dhidi ya dini tukufu ya Kiislamu.

Gérald Darmanin, waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, alidai jana Jumanne wakati alipohojiwa na gazeti la Le Figaro la nchi hiyo kwamba Paris imeamua kufunga Misikiti mingine 6 kwa sabu ya eti kukabiliana na misimamo mikali. Vile vile alisema, Paris imefikia uamuzi wa kuvunja jumuiya kadhaa za Kiislamu kwa madai ya kufanya tablighi za misimamo mikali.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, vitendo vya chuki vya serikali ya Ufaransa dhidi ya Waislamu vimeongezeka kwenye miezi ya hivi karibuni.

Emmanuel Macron, rais wa nchi hiyo ya Ulaya hivi karibuni kwa mara nyingine alitoa maneno ya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu akijigamba kuwa Ufaransa itaendelea kuchapisha vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.

Chuki hizo za waziwazi ya rais wa Ufaransa dhidi ya Waislamu zimelaaniwa vikali na Waislamu pamoja na wakuu na viongozi wa Kiislamu kote ulimwenguni.

Hadi hivi sasa Waislamu wa Ufaransa mara nyingine wamekuwa wakilalamikia vikali vitendo vya chuki na uadui, kushambuliwa misikiti na vituo vya Kiislamu nchini humo vitendo ambavyo vinachochewa kwa makusudi na serikali ya Paris kupitia matamshi kama hayo ya Emmanuel Macron.

(Visited 23 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!