Mkutano wa 34 wa Umoja wa Kiislamu mwaka huu umepangwa kufanyika kwa njia ya Intaneti katika eneo la Mashariki na Kusini Mashariki mwa Asia kuanzia siku chache zijazo.

Mkutano huo umepangwa kufanyika chini ya kaulimbiu ya “Ushirikiano wa Kiislamu katika Kukabiliana na Majanga na Mabalaa” katika eneo la Mashariki na Kusini Mashariki mwa Asia kwa kushirikiana taasisi mbalimbali za kijamii na watu muhimu wenye hadhi za kiserikali na binafsi. Maulamaa wa Kiislamu kutoka Malaysia, Indonesia, Ufilipino, Thailand, Japan, Singapore, Myanmar, Korea Kusini, Cambodia, China na Timor Mashariki wameshathibitisha kushiriki kwenye mkutano huo utakaofanyika kwa njia ya video kuanzia Oktoba 29 (Mwezi 12 Mfunguo Sita 1443 Hijria) hadi Novemba 3, 2020 (Mwezi 17 Mfunguo Sita 1443 Hijria).

Shikamaneni nyote na kamba ya Mwenyezi Mungu wala msifarikiane

Miongoni mwa mada zitakazozungumziwa kwenye mkutano huo ni uwezo mkubwa wa kiistratijia wa ulimwengu wa Kiislamu, mchango wa maulamaa na wasomi Waislamu katika vyombo vya habari vya ulimwengu wa Kiislamu katika kukabiliana na mabalaa, majanga na vitisho mbalimbali na kutumiwa vizuri fursa za Intaneti katika wakati huu wa kuenea ugonjwa wa COVID-19 na jinsi jamii za Kiislamu zinavyoweza kunufaika vizuri na fursa hizo.

Mkutano huo utakaoanza siku ya Alkhamisi ya Oktoba 29, 2020 utafanyika kwa kutumia application ya Zoom na utarushwa moja kwa moja pia kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.

(Visited 21 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!