Manispaa ya Istanbul Uturuki imenunua nakala 9 za kurasa za kale za Qur’ani Tukufu zilizoandikwa kwa mkono na athari nyingine za sanaa kutoka katika mnada wa Sotheby’s wa mjini London, UIngereza.

Toleo la mtandaoni la gazeti la serikali la Daily Sabah la nchini Uturuki limeripoti kuwa, mbali na nakala 9 za kurasa za kale za Qur’ani Tukufu zilizoandikwa kwa mkono, manispaa hiyo imenunua ‘athar’ nyingine za Kiislamu na kihistoria katika mnada huo.

Gharama za ‘athar’ hizo hazikutangazwa, lakini zinajumuisha pia picha nadra ya Suleiman I (Suleiman the Magnificent), mfalme wa utawala wa Uthmania (Ottoman Empire) wa karne ya 16 ambaye utawala wake ndio uliokuwa mrefu zaidi kuliko tawala zote za wafalme wa silisila hiyo. Alitawala baina ya mwaka 1520 hadi 1566 Milaadia. Meya wa Istanbul, Ekrem İmamoğlu, ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba: “Katika mnada wa leo (Jumamosi, Aprili 3, 2021) tumenunua nakala 9 za kale zilizoandikwa kwa mkono za Qur’ani Tukufu na vitabu vingine zikiwemo kurasa za Qur’ani Tukufu zilizoandikwa miaka 700 (karne saba) iliyopita na ndani yake mna Sura tano na pia ukurasa wa miaka 1100 iliyopita wenye sura ya al Maidah na kurasa za miaka 1200 iliyopita zenye sura ya al Zukhruf.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!