Mamia ya Wapalestina, Jumamosi, Aprili 10, 2021 walishiriki katika zoezi la kuuosha na kuusafisha Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu ikiwa ni katika maandalizi ya kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hayo yameripotiwa na gazeti la al Quds al Arabi ambalo limesema kuwa, mamia ya Wapalestina, wakubwa kwa wadogo wameshiriki katika zoezi la kuusafisha na kuuosha Msikiti Mtakatifu wa al Aqsa ikiwa ni sehemu ya ibada za kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Ghazi Isa, mkuu wa asasi ya kiraia ya “Jam’iyyat al Ighatha 48” amesema kuwa, siku ya Jumamosi, Wapalestina kutoka kona mbalimbali za ardhi hizo walifika katika Kibla cha Kwanza cha Waislamu kwa kutumia njia mbalimbali, ili kushiriki katika zoezi hilo la kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu. Hiyo ni sehemu ya kampeni maalumu huko Palestina inayojulikana kwa jina la “Quds Kwanza.” Kwa mujibu wa mkuu wa asasi hiyo ya kiraia, kampeni hiyo inafanyika kwa muda wa miaka 12 sasa.

Hapa chini tumeweka kipande kifupi cha video cha zoezi hilo

(Visited 74 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!