Msikiti wa kwanza wa sola (unaotumia nguvu za jua) ambao unachunga mazingira na unapunguza sana gharama za umeme msikitini, umefunguliwa katika mji mkuu wa Kazakhstan, Nur-Sultan (Astana).

Televisheni ya al Alam imeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, Nur-Sultan, mji mkuu wa Kazakhstan umeshuhudia kufunguliwa msikiti wa kwanza unaochunga vizuri mazingira kutokana na kutumia kwake nishati ya jua kuzalisha umeme.

Wakuu wa mji huo wameamua kuupa msikiti huo sahani za kufyonza nguvu za jua na kuzihifadhi ndani yake kwa ajili ya kuzalisha umeme msikitini humo ili mbali na kuchunga mazingira, teknolojia hiyo iweze kupunguza sana gharama za matumizi ya umeme. Hivi sasa sahani hizo za sola zinazalisha umeme mara tatu zaidi ya unaohitajika msikitini humo.

Sheikh Yahya Kaji ambaye ndiye Imam wa msikiti huo ambao wakazi wa eneo hilo wanauita kwa jina la “Ua la Allah”   amesema, msikiti huo umejengwa kwa kujitolea wakazi wa mji wa Nur-Sultan. Kazakhstan ni nchi ya katikati mwa Asia. Ni miongoni mwa jamhuri za Urusi ya zamani zilizojitenga mwaka 1991. Ilitawaliwa na Umoja wa Kisovieti (Urusi ya zamani) kuanzia mwaka 1936. Wengi wa wakazi wa nchi hiyo ni Waislamu.

(Visited 54 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!