Msikiti wa al Aqsa, Kibla cha Kwanza cha Waislamu, kimefunguliwa katika siku ya kwanza ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani wa 1442 Hijria kwa ajili ya Waislamu wote wa Palestina. Ikumbukwe kuwa, Msikiti huo mtakatifu haukuwa wazi kutokana na mazingira magumu ya ugonjwa wa COVID-19.

Kwa mujibu wa tovuti ya “Arabi 21” Waislamu wenye saumu wa Palestina wamefarijika na kufurahi mno kuona sasa wanaweza kutekeleza ibada zao ndani ya Msikiti huo katika mwezi huu wa Ramadhani wakimuomba Mwenyezi Mungu aliondoe duniani janga hili la COVID-19.

Tangu Idara ya Wakfu wa Kiislamu ya Quds ilipotangaza habari hiyo, mamia ya Waislamu wamekwenda kufanya ibada Msikiti hapo. Kabla ya hapo pia Waislamu hao walishiriki kwa mamia katika usafi wa eneo hilo takatifu kama sehemu ya kuukaribisha kiibada mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Siku kadhaa nyuma, vijana wa Palestina walizipamba barabara, mitaa na vichochoro  vya karibu na Msikiti wa al Aqsa, kwa mataa na mapambo mbalimbali kama sehemu ya kudhihirisha furaha yao kuu ya kuona Msikiti huo umefunguliwa.

Pamoja na furaha hiyo, lakini mateso ya Waislamu wa Palestina bado yapo. Shirika la habari la WAFA la Palestina Jumatatu usiku lilitangaza kuwa, wanajeshi wa Israel waliwashambulia vijana wa Palestina wakati walipokuwa wanarudi kusali Tarawehe katika Msikiti wa al Aqsa.

Hapa chini tumeweka kipande cha video kuhusu hali ya Msikiti wa al Aqsa katika mwezi huu wa Ramadhani.

Na hapa chini ni baadhi ya picha za Waislamu wa Palestina wakisali katika eneo hilo takatifu.

(Visited 1 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!