Msikiti wa Lala Tulpan ulioko mjini Ufa, makao makuu ya Jamhuri ya Bashkortostan nchini Russia ni moja ya misikiti mikubwa zaidi nchini Russia na ni maarufu kwa muundo wake wa kipekee na usanifu majengo wa aina yake.

Msikiti wa Lala Tulpan ni moja ya vivutio vikubwa vya utalii katika mji huo wa Ufa. Msikiti huo una minara pacha yenye urefu wa mita 53 kila mmoja. Ni mkubwa kiasi cha kuweza kupokea hata Waislamu 1000 kwa wakati mmoja kwa ajili ya Sala ya jamaa.

Msikiti huo ulianza kujengwa mwaka 1990 na ujenzi wake ulimalizika mwaka 1998. Mchoraji wa ramani ya Msikiti huo ni Wakil Davlyatshin. Msikiti wa Lala Tulpan ulizidi kupata umaarufu kutokana na kufanyika mkutano maalumu baina ya Rais Vladimir Putin wa Russia na maulamaa wa Kiislamu wa nchi hiyo.

Hapa chini tumeweka video fupi ya Msikiti huo

Na hapa chini ni baadhi ya picha za Msikiti huo

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!