Sheikh Niurin Muhammad Siddiq, qarii maarufu wa Sudan amefariki dunia katika ajali ya barabarani pamoja na maqarii wenzake watatu wakubwa.

Mtandao wa Kiarabu wa televisheni ya al Jazeera ya Qatar umeripoti habari hiyo na kunukuu ujumbe wa Facebook uliosambazwa na Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kidini wa Sudan, Nasruddin Mofarih  akisema kuwa, maqarii wakubwa wa Qur’ani tukufu, Masheikh Nourin Muhammad Siddiq,  Ali Yaaqoub, Abdallah Awadh al Karim na Mohannad al Kanani wamefariki dunia katika ajali ya barabarani nchini Sudan.

Amesema, Sayyid bin Omar, qarii mwingine wa Misri amejeruhiwa katika ajali hiyo na amelazwa hostpitalini.

Kwa upande wake, Mohamed Hamdan Dagalo (Hemedti), Makamu wa Rais wa Baraza la Uongozi la Sudan ametoa mkono wa pole kufuatia ajali hiyo na kufariki dunia maqarii hao wakubwa wa Qur’ani Tukufu. Amesema, Sheikh Nourin Muhammad Siddiq na wenzake wamefariki dunia katika ajali ya barabarani wakati walipokuwa wanarejea nyumbani kutoka kwenye mwaliko wa kusoma Qur’ani Tukufu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Sudan, ajali hiyo imetokea katika umbali wa kilomi 18 kutoka mji wa Omdurman, magharibi mwa Mto Nile.

Sheikh Nourin Muhammad Siddiq amepata umaarufu kutokana na qiraa zake nzuri kwa kutumia lahani tofauti ikiwemo usomaji wa tartili kwa lahaja ya Kisudan kama anavyoonekana kwenye video hii hapa chini. Alikuwa Imam wa Msikiti maarufu zaidi wa Khartoum, mji mkuu wa Sudan.

Angalia kipande cha video hiki hapa chini. Sheikh Nourin Muhammad Siddiq anasoma kwa khushuu ya hali ya juu huku akibubujikwa na macho.

Innaa Lillahi Wainna Ilayhi Raajiun.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!