Usiku wa tarehe 15 Shaabani ni usiku mtukufu kwa wakaazi wa kusini mwa Iran na katika visiwa vya Ghuba ya Uajemi. Unaitwa ni usiku wa Helheluwa.

Katika mji wa Bandar Kong, kila mwaka baada ya Sala ya Magharibi hadi saa tatu usiku, watoto hupita nyumba moja moja na hugonga milango huku wakiimba nyimbo mahsusi. Wenye nyumba huwapa watoto maperemende, biskuti au haluwa.

Utamaduni huu bado unaendelea, hasa katika mji wa Kong ambao ni mji mkongwe wa mabaharia ambao takriban wazee wote katika mji huo wanazungumza Kiswahili kutokana na misafara yao kwa majahazi katika upwa wa Uswahilini na visiwa vya Zanzibar na Lamu.

Hapa chini tumeweka video fupi ya sherehe hizo

(Visited 55 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!