Wakazi wa kijiji kimoja cha kaskazini mwa Misri wamefanya maandamano katika maeneo tofauti ya kijiji hicho ili kuwaenzi vijana 115 waliohifadhi Qur’ani nzima wakiwemo watoto wadogo 80.

Mtandao wa habari wa “ahlmasrnews” umeripori habari hiyo pamooja na mkanda wa video na kuongeza kuwa, wakazi wa kijiji cha al Riyadh cha mji wa Nasr mkoa wa Beni Suef walifanya sherehe hizo siku ya Ijumaa kwa ajili ya kuwaenzi vijana 115 waliohifadhi Qur’ani Tukufu. Vijana wa rika na umri tofauti wakiwemo watoto wadogo 80 ni miongoni mwa walioenziwa kwa kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

Vijana hao wamevishwa mavazi maalumu vikiwemo vitambaa virefu vilivoandikwa mahuffadh wa Kitabu cha Mwenyezi Munngu. Vijana hao wametembezwa kwenye mitaa na vichochoro vya kijiji hicho wakimsalia Mtume na kupiga takbiri huku wakipongezwa na wanakijiji.

Maandamano ya kuwaenzi na kuwapongeza wanaohifadhi Qur’ani Tukufu ni ada na desturi ya zamani katika baadhi ya nchi za Kiarabu na hufanyika kwa ajili ya kuwahamasisha watu kuhifadhi aya za Kitabu hicho kitakatifu.

Hivi karibuni pia katika mji wa Ghaza huko Palestina kulifanyika maandamano kama hayo kwa ajili ya kuwaenzi waliohifadhi Qur’ani Tukufu.

(Visited 22 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!