Msikiti Mkuu wa al Mardzhani Kazan wa Waislamu wa Jamhuri ya Tatarstan nchini Russia umekuwa mwenyeji wa kikao cha viongozi wa Kiislamu kutoka kona zote za nchi hiyo. Kikao hicho kimefanyika chini ya kaulimbiu ya “Halali, Mtindo Bora wa Kuishi.”

Mtandao wa “Realnoe Vremya” umeripoti habari hiyo na kusema kuwa, washiriki katika kikao hicho kilichofanyika ndani ya Msikiti Mkuu wa mji wa Kazan ambayo ndiyo makao makuu ya Jamhuri ya Tatarstan huko Russia wamejadiliana njia za kuweza kustawisha na kueneza mtindo wa Kiislamu wa Waislamu wa kula vyakula vya halali ikiwa ni pamoja na kuwasaidia Waislamu wenye upungufu wa viuongo kupata kiurahisi vyakula hivyo. Na pia kuweza Waislamu kupata huduma za Kiislamu na kuishi kwa mujibu wa mafundisho ya dini yao.

Viongozi wa Waislamu wa Russia katika kikao cha kujadili njia za kuishi Kiislamu

Bi Taliya Minullina, Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Uwekezaji ya Russia amesema kuwa, mzunguko wa fedha za uchumi wa Kiislamu duniani sasa hivi umefikia dola bilioni 5 kwa mwaka na kiwango hicho kitaongezeka kwa zaidi ya mara moja na nusu ifikapo mwaka 2024.

Amesema, nchini Russia kuna vituo vingi vya kutoa vibali vya chakula cha halali ambapo Kamati ya Viwango vya Vyakula Halali katika Baraza la Waislamu wa Jamhuri ya Tatarstan ni moja ya vituo hivyo.

Bi Taliya Minullina ameongeza kuwa, kongamano la pamoja la Waislamu wa Russia na nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC hufanyika kila mwaka likiwajumuisha pamoja mamia ya wanadiplomasia, wataalamu, wazalishaji bidhaa na waajiri wanaojishughulisha na masuala ya ustawi wa uchumi wa Kiislamu. Kongamano hilo hufanyika mjini Kazan, Jamhuri ya Tatarstan nchini Russia kila mwaka. Hata hivyo kongamano hilo halikufanyika mwaka huu kutokana na maambukizi ya kirusi cha corona na kuenea ugonjwa wa COVID-19. Kongamano lijalo limepangawa kufanyika mwezi Julai 2021.

Sheikh Mansour Jalaluddin, Mkuu wa Baraza la Watu Wazima wa Kazan ambaye pia ni Imam wa Msikiti Mkuu wa mji huo amesema kwamba, suala la halali haliishii tu katika vyakula, bali linajumuisha pia madawa, utalii na katika masuala mengine yote.

Amesikitika kusema kuwa, watalii Waislamu wanaotembelea Russia wanalazimika kwenda maeneo ya mbali kutafuta chakula cha halali na kwa kawaida hawapati huduma za halali zinazochunga mafundisho ya dini yao.

Hata hivyo amesema, Jamhuri ya Tatarstan imepiga hatua nzuri hivi sasa, ina mikahawa mingi, mahoteli, maeneo ya starehe na vituo vingi vya afya vinavyochunga mafundisho ya Uislamu.

(Visited 22 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!