Serikali ya Sri Lanka imeanzisha kampeni maalumu ya kutangaza vivutio vya Kiislamu na chakula halali ili kuongeza idadi ya watalii wa kigeni wanaotembelea nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Asia.

Sri Lanka iko kwenye eneo zuri la kijiografia na ndio maana linavutia watalii wengi wa kigeni. Lakini kuna baadhi ya mambo yanawafanya watalii waone tabu kutembelea nchi hiyo, miongoni mwake ni watu wake kutojikinga na najisi na pia kukosekana chakula halali hasa kwa watalii Waislamu.

Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Colombo, mji mkuu wa Sri Lanka imeanzisha kampeni maalumu ya kutanua wigo wa sekta yake ya utalii kupitia kutangaza vivutio vingi vya Kiislamu pamoja na chakula halali (Halal Food).

Mabaharia Waislamu walifika karne nyingi nyuma nchini Sri Lanka kutokana na nchi hiyo kuwa katika eneo zuri sana la kijiografia kiasi kwamba moja ya majina ya kale ya kisiwa hicho cha Sri Lanka ni Serendib lenye asili ya Kiarabu. Hivi sasa idadi ya Waislamu nchini Sri Lanka ni asilimia 9.4 na ijapokuwa ni katika jamii ya wachache, lakini wanaunda asilimia kubwa zaidi ya raia wa nchi hiyo baada ya wale wa dini kuu ya kibudha. Wengi wa Waislamu wa Sri Lanka wana asili ya Morocco ambao ni maarufu pia kwa jina la Moors.

(Visited 34 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!