Wabunge wa Bunge la Jimbo la Sindh Pakistan wamewawasilisha muswada katika bunge hilo na kutaka Qur’ani Tukufu liwe somo la lazima kwa taasisi zote za elimu za jimbo hilo.

Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa “The News” wabunge wa bunge hilo kutoka chama cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) wamewasilisha muswada bungeni wakitaka masomo ya Qur’ani Tukufu yawe ya lazima kwa kila taasisi ya elimu ya jimbo hilo la kusini mashariki mwa Pakistan.

Muswada wa sheria hiyo uliwasilishwa bungeni hapo hivi karibuni na wabunge watatu wa chama cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) ukiwa na jina la “Masomo ya Lazima ya Qur’ani 2021.” Wabunge hao ni Shahzad Qureshi, Rabia Azfar na Arsalan Taj. “Wamewasilisha muswada huo baada ya kupasishwa na Mufti Taqi Usmani,” imeendelea kusema ripoti hiyo.

Ikumbukwe kuwa, kuanzia mwaka jana, Qur’ani ilianza kuwa somo la lazima kwa vyuo vikuu vyote vya jimbo la Punjab ambalo ndilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu kuliko majimbo mengine yote ya Pakistan.

(Visited 38 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!