Raia 16 elfu wa Saudi Arabia pamoja na wageni waishio nchini humo wametumia application ya kujiandikisha kwa ajili ya ibada ya Umra katika hatua ya awali ya uandikishaji huo.

Gulf Businnes

Kwa mujibu wa “Gulf Business” uandikishaji wa Umra umemalizika kwa ajili ya siku 10 za awali.

Liwali wa Makkah amethibitisha hayo katika ujumbe wake alioutuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Ibada ya Umra na ziara katika Misikiti Miwili Mitakatifu itafanyika kwa awamu mwaka huu kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Awamu za Umra na Ziara

Vyombo vya habari vya Saudi Arabia vimeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, awamu ya kwanza ya Umra na ziara ya Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makkah na Madina, itafanyika kwa ajili ya raia wa Saudia na wageni wanaoishi nchini humo na itaanza tarehe 4 Oktoba 2020. Kila siku Waislamu 6,000 yaani asilimia 30 ya kiwango kilichoainishwa kutokana na corona, watafanya ibada hiyo.

Waislamu katika ibada ya Sala nchini Saudi Arabia

Awamu nyinginezo

Awamu ya pili itaanza tarehe 18 Oktoba kwa raia na wageni wanaoishi Saudia na kwa siku Waislamu 15,000 watafanya ibada ya Umra na 40,000 watatekeleza ibada ya Sala, idadi ambayo itakuwa ni asilimia 75 ya kiwango kilichoainishwa wakati huu wa corona. Katika awamu ya tatu pia ambayo itaanza tarehe Mosi Novemba, 2020 hadi itakapotangazwa rasmi kumalizika maambukizo ya corona na hali kurejea kama ilivyokuwa zamani, watakaoendelea kuruhusiwa kufanya ibada ya Umra watakuwa ni raia na wageni waishio ndani ya Saudi Arabia.

Umra kwa waishio nje ya Saudia

Hata hivyo watu kutoka nje ya Saudi Arabia nao wataruhusiwa kufanya ibada hiyo lakini kwa siku watakuwa ni Waislamu 20,000 wa ibada ya Umra na 60,000 wa kutekeleza ibada ya Sala na ziara katika Nyumba ya Allah. Idadi hiyo itakuwa ni asilimia 100 ya kiwango kilichoanishwa katika kipindi hiki cha ugonjwa wa COVID-19.

(Visited 11 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!