Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini Italia (UCOII) umeanzisha mfuko maalumu wa kukusanya fedha kwa ajili ya kuasisi kanali ya kutoa taarifa za kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu nchini humo.

Mtandao wa habari wa Arab News umeripoti kuwa, UCOII imefungua mfuko maalumu kwa ajili ya kuanzisha mtandao huo wa kupambana na chuki dhidi ya Uislamu nchini Italia unaojullikana kwa jina la NIA. 

Kanali hiyo itakuwa inakusanya ripoti zinazohusiana na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu kupitia tovuti maalumu na wataalamu tofauti.

Kanali hiyo itatanua pia wigo wa mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu huko Italia.

Uchunguzi uliofanywa na Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini Italia (UCOII) unaonesha kuwa, asilimia 65 ta Waislamu wa nchi hiyo wanakumbwa na ukandamizaji, taasubu na ubaguzi kutoka watu na taasisi mbalimbali.

Uchunguzi huo unaonesha kuwa, wanawake Waislamu ndio wahanga wakubwa wa vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu nchini Italia. Kwa mfano, kama wanawake Waislamu watavaa vazi la staha la Hijab, jambo hilo litaoneshwa ni kioja kikubwa na watakejeliwa na vyombo vingi vya habari. Zaidi ya hayo ni kwamba Wanawake Waislamu nchini Italia wanapata tabu sana ya kuajiriwa.

(Visited 29 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!