Wahanga wakuu wa mgogoro wa Kongo ni raia wa kawaida

Watu wasiojulikana wenye silaha Jumatatu wameshambulia vijiji vitatu katika mkoa wa Ituri wa kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuua wanavijiji 19 wakiwemo wanawake na watoto wadogo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, watu wenye silaha wasiojulikana, wameshambulia vijiji vya Lisey, Tchulu na Aloys vya mkoa wa Ituri na kuua wanavijiji watano, wawili na 12 kwa utaratibu wa vijiji hivyo.

Maeneo ya kaskazini, mashariki na kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamekuwa ni uwanja wa machafuko kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

Udhaifu wa jeshi la serikali na askari wa kofia buluu wa Umoja wa Mataifa ambao wameshindwa kumaliza makundi ya waasi ni miongoni mwa sababu kuu za kuendelea machafuko na ukosefu wa utulivu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!