Makumi ya maelfu ya Wapalestina wameshiriki katika Sala ya leo ya Ijumaa iliyosaliwa kwenye Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu licha ya wanajeshi na askari wa Israel kuweka masharti magumu ya kuwazuia wasifike kwenye Msikiti huo mtakatifu.

Kwa mujibu wa Kituo cha Upashaji Habari cha Palestina (PIC), zaidi ya Wapalestina 45 elfu wameshiriki kwenye Sala ya Ijumaa iliyosaliwa ndani na nje ya Msikiti wa al Aqsa.

Maelfu ya Wapalestina wanaoishi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu tangu mwaka 1948 wametumia njia mbalimbali kuhakikisha wanafikka Msikitini hapo mapema leo asubuhi.

Khatibu wa Msikiti wa al Aqsa, Sheikh Mohammed Sarandah amesema katika khutba zake kwamba, Wapalestina daima wako kwenye medani ya mapambano na Mlinzi wa Msikiti huo mtakatifu yaani Allah ametoa bishara njema kwamba Siku ya Kiyama wanaopigana katika njia ya Mwenyezi Mungu watakuwa na mafanikio na mwisho mwema.

Amesema, Wapalestina ambao muda wote wako pamoja na Msikiti wa al Aqsa, Siku ya Kiyama Allah atawalipa malipo bora kutokana na kuvumilia kwao kila aina ya mateso na tabu. Vile vile amewashukuru na kuwapongeza wanafunzi na walimu wao ambao muda wote hawaondoki kwenye Kibla hicho cha Kwanza cha Waislamu. 

Idadi hiyo kubwa ya Waislamu wameshiriki katika Sala ya Ijumaa pamoja na kwamba wanajeshi wa utawala wa Kizayuni lwameweka ulinzi mkali zaidi katika kona mbalimbali za mji mtukufu wa Baytul Muqaddas (Quds) ili kuzuia Waislamu wasijitokeze kwa wingi kwenye Sala ya Ijumaa.

Wanajeshi hao vile vile wamewazuia Wapalestina wengi wasiingie katika mji wa Quds sawa kabisa na wanavyowafanyia Wapalestina siku zote.

(Visited 1 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!