Mashindano ya 35 ya Qur’ani Tukufu yalimalizika Jumamosi, Machi 27, 2021 kwa kupewa zawadi washindi wa mashindano hayo.

Kwa mujibu wa “Tribune Online” mashindano hayo yalifanyika kwa muda wa siku 9 katika jimbo la Kano la kaskazini mwa Nigeria.

Dk. Nasiru Gawuna, Naibu Mkuu wa Mkoa wa Kano amehutubia hadhirina katika sherehe za kufunga mashindano hayo na huku akigusia jinsi washiriki kutoka majimbo 36 ya Nigeria walivyochuana vikali katika mashindano hayo amesema, washiriki 180 wanaume na 190 wanawake wamechuana kwenye mashindano hayo.

Dk Gawuna amewashukuru washiriki wote wa mashindano hayo na kutilia mkazo umuhimu wa kuendeleza mashindano ya Qur’ani na kueneza utamaduni wa hifdh na qiraa katika ngazi na daraja tofauti.

Muhammad Auwal Gusau kutoka jimbo la Zamfara ndiye aliyeibuka mshindi kati ya washindani wanaume na Nusaiba Shu’aibu Ahmed kutoka jimbo la Kano ndiye aliyeibuka na ushindi upande wa wanawake katika mashindano hayo ya 35 ya Qur’ani Tukufu ya nchini Nigeria. Kila mmoja wa washindi hao wawili wa kwanza amepewa zawadi wa Naira milioni 2 na laki 5 za Nigeria sawa na takriban dola 6,700 za Kimarekani.

(Visited 47 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!