Mtandao wa habari wa al Yaum al Sab’i umeripoti kuwa, Idara ya Wakfu ya Mkoa wa Giza wa pembeni mwa Mto Nile imetoa amri ya kupigwa dawa misikiti yote mkoani humo kama sehemu ya kupambana na kirusi cha corona. Tayari zoezi hilo limeanza katika kona zote za mkoa huo.

Sayyid Mas’ad, Mkurugenzi wa Wakfu mkoani Giza, Misri amesema, hayo ni katika kutekeleza amri ya Waziri wa Wakufu wa nchi hiyo ili kuhakikisha kwamba Waislamu wanashiriki katika ibada misikitini bila ya wasiwasi wa kuambukiwa ugonjwa wa COVID-19. Hapa chini tumeweka baadhi ya picha chache za zoezi hilo:

Usafi ni katika imani

Mkoa wa Giza nchini Misri ukiendesha zoezi la kupiga dawa misikiti kukabiliana na corona.

(Visited 8 times, 1 visits today)

Leave a Reply

Your email address will not be published.

error: Content is protected !!